Title: The Holy Bible: Swahili New Testament


download 3.63 Mb.
jenengTitle: The Holy Bible: Swahili New Testament
Kaca1/69
KoleksiTest
k.kabeh-ngerti.com > Tengen > Test
  1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   69
__________________________________________________________________
Title: The Holy Bible: Swahili New Testament

Creator(s): Anonymous

Language:

Rights: Public Domain

CCEL Subjects: All; Bible; New Testament

__________________________________________________________________
Holy Bible
Swahili New Testament

__________________________________________________________________
New Testament

__________________________________________________________________
Matthew

__________________________________________________________________
Chapter 1
^1Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi, mzawa wa Abrahamu. Hii ndiyo

orodha ya ukoo wake:
^2Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na

ndugu zake,
^3Yuda alimzaa Faresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Faresi alimzaa

Hesroni, Hesroni alimzaa Rami,
^4Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa

Salmoni,
^5Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu). Boazi na

Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi, Obedi alimzaa Yese,
^6naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake

Solomoni alikuwa mke wa Uria).
^7Solomoni alimzaa Rehoboamu, Rehoboamu alimzaa Abiya, Abiya alimzaa

Asa,
^8Asa alimzaa Yehoshafati, Yehoshafati alimzaa Yoramu, Yoramu alimzaa

Uzia,
^9Uzia alimzaa Yothamu, Yothamu alimzaa Ahazi, Ahazi alimzaa Hezekia,
^10Hezekia alimzaa Manase, Manase alimzaa Amoni, Amoni alimzaa Yosia,
^11Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake. Huo ulikuwa wakati Wayahudi

walipopelekwa uhamishoni Babuloni.
^12Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni: Yekonia alimzaa

Shealtieli, Shealtieli alimzaa Zerobabeli,
^13Zerobabeli alimzaa Abiudi, Abiudi alimzaa Eliakimu, Eliakimu alimzaa

Azori,
^14Azori alimzaa Zadoki, Zadoki alimzaa Akimu, Akimu alimzaa Eliudi,
^15Eliudi alimzaa Eleazeri, Eleazeri alimzaa Mathani, Mathani alimzaa

Yakobo,
^16Yakobo alimzaa Yosefu, aliyekuwa mume wake Maria, mama yake Yesu,

aitwaye Kristo.
^17Basi, kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi,

vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka

Babuloni, na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati

wa Kristo.
^18Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake,

alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na

mke, alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
^19Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha

hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.
^20Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika

ndoto, akamwambia, "Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria

awe mke wako, maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
^21Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye

atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao."
^22Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa

njia ya nabii:
^23"Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, naye ataitwa

Emanueli" (maana yake, "Mungu yu pamoja nasi").
^24Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo

alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani.
^25Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa

kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.

__________________________________________________________________
Chapter 2
^1Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode

alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota

kutoka mashariki walifika Yerusalemu,
^2wakauliza, "Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa?

Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu."
^3Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi

wote wa Yerusalemu.
^4Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria,

akawauliza, "Kristo atazaliwa wapi?"
^5Nao wakamjibu, "Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii

alivyoandika:
^6`Ewe Bethlehemu katika nchi ya Yuda, kwa vyovyote wewe si mdogo

kabisa kati ya viongozi wa Yuda; maana kwako atatokea kiongozi

atakayewaongoza watu wangu, Israeli."`
^7Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza

wakati hasa ile nyota ilipowatokea.
^8Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, "Nendeni mkachunguze kwa makini

habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende

nikamwabudu."
^9Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe

ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata

ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
^10Walipoiona hiyo nyota, walifurahi mno.
^11Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama

yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao,

wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane. ic
^12Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode; hivyo wakarudi

makwao kwa njia nyingine.
^13Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu

katika ndoto, akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake,

mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokwambia, maana Herode

anakusudia kumwua huyu mtoto."
^14Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake,

akaondoka usiku, akaenda Misri.
^15Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno

alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: "Nilimwita Mwanangu kutoka

Misri."
^16Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa

wamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuru watoto wote wa kiume mjini

Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake

wauawe. Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale

wataalamu wa nyota.
^17Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia:
^18"Sauti imesikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli

anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki."
^19Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika

ndoto kule Misri,
^20akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena

katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo

wamekwisha kufa."
^21Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea

katika nchi ya Israeli.
^22Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa

mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada

ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya,
^23akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno

yaliyonenwa kwa njia ya manabii: "Ataitwa Mnazare."

__________________________________________________________________
Chapter 3
^1Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa

la Yudea:
^2"Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia."
^3Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema:

"Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake,

nyoosheni vijia vyake."`
^4Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa

ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
^5Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu

zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
^6wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
^7Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili

awabatize, aliwaambia, "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea

kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
^8Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
^9Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, `Baba yetu ni

Abrahamu!` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe

watoto wa Abrahamu.
^10Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti

usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
^11Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini yule

anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hata kubeba

viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
^12Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka

yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika."

ic
^13Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani,

akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
^14Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, "Je, wewe unakuja kwangu?

Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe."
^15Lakini Yesu akamjibu, "Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna

hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka." Hapo Yohane

akakubali.
^16Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu

zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu

yake.
^17Sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa,

nimependezwa naye."

__________________________________________________________________
Chapter 4
^1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
^2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
^3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu,

amuru mawe haya yawe mikate."
^4Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu

hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."`
^5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka

juu ya mnara wa hekalu,
^6akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana

imeandikwa: `Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua

mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."`
^7Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: `Usimjaribu Bwana, Mungu wako."`
^8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme

zote za ulimwengu na fahari zake,
^9akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na

kuniabudu."
^10Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: `Utamwabudu

Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."`
^11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
^12Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.
^13Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya

Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
^14Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
^15"Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng`ambo ya

mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
^16Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika

nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!"
^17Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana

ufalme wa mbinguni umekaribia!"
^18Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu

wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa

wakivua samaki kwa nyavu ziwani.
^19Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa

watu."
^20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ic
^21Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na

Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba

yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,
^22nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
^23Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha

katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu.

Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
^24Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye

maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu:

waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa,

walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
^25Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea

na ng`ambo ya mto Yordani, walimfuata.

__________________________________________________________________
Chapter 5
^1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda mlimani, akaketi. Wanafunzi

wake wakamwendea,
^2naye akaanza kuwafundisha:
^3"Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
^4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
^5Heri walio wapole, maana watairithi nchi.
^6Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana

watashibishwa.
^7Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.
^8Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.
^9Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.
^10Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme

wa mbinguni ni wao.
^11"Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia

kila aina ya uovu kwa ajili yangu.
^12Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo

ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
^13"Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake

itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na

watu.
^14"Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi

kufichika.
^15Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa chungu, ila huiweka juu ya

kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani.
^16Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili

wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni."
^17"Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua Sheria ya Mose na mafundisho ya

manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha.
^18Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna

hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka

yote yametimia.
^19Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na

kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika

Ufalme wa mbiguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine,

huyo atakuwa mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
^20Ndiyo maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa Mafarisayo na

walimu wa Sheria, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
^21"Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: `Usiue! Atakayeua

lazima ahukumiwe.`
^22Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima

ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita

ndugu yake: `Pumbavu` atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
^23Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka

kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe,
^24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na

ndugu yako, ndipo urudi ukatoe sadaka yako.
^25"Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani, kwenda mahakamani.

La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu

atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani.
^26Kweli nakwambia, hutatoka humo mpaka umemaliza kulipa senti ya

mwisho.
^27"Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: `Usizini!`
  1   2   3   4   5   6   7   8   9   ...   69

Share ing jaringan sosial


Similar:

*Title inspired by Frank Sinatra's song of the same name

Additional file 2 Searched Papers Containing pm in Title/Abstract 2012

A freelance translator with B. Eng title and working experience as environmental consultant”

Kimia


Nalika Nyalin materi nyedhiyani link © 2000-2017
kontak
k.kabeh-ngerti.com
.. Home